Msaada
Gripa Music
paroles Gripa Music Msaada

Gripa Music - Msaada Lyrics & Traduction

Kimbilio langu
Msaada wangu wa karibu ni wewe
Tegemeo langu
Tumaini la maisha yangu ni wewe

Pale ninaposhindwa kupata msaada
Nitainua macho yangu nitazame milima
Msaada wangu si kwa mwanadamu
Wala msaada wangu si kwa elimu yangu

Msaada wangu, u katika Bwana
Yeye aliyefanya mbingu na dunia
Msaada wangu, u katika Bwana
Yeye aliyefanya mbingu na dunia

Akili zangu zinapofika mwisho
Uso nimelemewa na uzisho
Hapo ndipo Mungu huleta suluhisho
Maishani

Maana wewe si mwepesi wa hasira
Lakini wewe wewe umejawa nguvu
Upitapo huzuka kimbunga na dhuruba
Na mawingu, ni vumbi litimuliwalo kwa nyayo zako

Wewe ni mwema
Wewe ni ngome ya usalama wakati wa taabu
Maana wewe si mwepesi wa hasira
Lakini wewe wewe umejawa nguvu

Maana msaada wangu si kwa mwanadamu
Wala msaada wangu si kwa elimu yangu

Msaada wangu, u katika Bwana
Yeye aliyefanya mbingu na dunia
Msaada wangu, u katika Bwana
Yeye aliyefanya mbingu na dunia

Msaada wangu, u katika Bwana
Yeye aliyefanya mbingu na dunia
Msaada wangu, u katika Bwana
Yeye aliyefanya mbingu na dunia

(Nguvu yangu ni wewe)

Msaada wangu, u katika Bwana
Yeye aliyefanya mbingu na dunia

Oh oh, oh-oh-oh-oh
Oh oh, oh-oh-oh-oh


Paroles2Chansons dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)