Mambo Yamebadilika
Martha Mwaipaja
paroles Martha Mwaipaja Mambo Yamebadilika

Martha Mwaipaja - Mambo Yamebadilika Lyrics & Traduction

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yangu si vile, neema imeniona
Mambo yamebadilika, eleza ya leo

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa

Wewe ni kila kitu Yesu, asante
No no no no, nimetazamwa na mimi
Hallelujah Mungu amenitoa mbali na mimi
Wakati kuzimu ilipanga kila siku nilie
Ndivyo mbingu ilipanga na mimi nifurahi

Ilipochimbwa shimo nizame nisitoke tena
Hivyo mbingu ilipanga nitatoka namna gani
Ni vile hukujua na mimi napendwa na Mungu
Hukutambua na mimi nimedhaminiwa

Ulieleza mabaya kila ulipopita
Naomba leo tangaza haya mema
Waambie watu Mungu si mwanadamu
Waambie amejawa na huruma
Waambie watu Mungu ni wa wote kweli
Waambie hana upendeleo kabisa
Usiwaambie watu mambo mabaya mabaya
Jifunze kusema mambo yaliyo mema

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa

Usiwaambie watu yule ni masikini tu
Waambie sasa wameshabarikiwa
Usiwaambie watu yule ni mama mjane tu
Waambie Yesu ni mume wa wajane

Usiwaambie yule ni mtoto wa yatima tu
Waambie Mungu ni baba wa mayatima
Usiwaambie watu yule ni mgonjwa namjua
Waambie Mungu anaponya kila kitu

Usiwaambie yule namjua ni wa chini sana
Waambie sasa ameshainuliwa
Usiwaambie yule ni masikini namjua
Waambie ameshabarikiwa

Usiwaambie mambo ya jana rafiki
Jifunze kusema mambo ya leo hii
Ya kale yamepita rafiki elewa tu
Sasa yamekuwa mapya nimeshasaidiwa

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yangu si vile, neema imeniona
Mambo yamebadilika, eleza ya leo

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yangu si vile, neema imeniona
Mambo yamebadilika, eleza ya leo

Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa
Mambo yamebadilika, mambo yamebadilika
Ukieleza mambo yangu, eleza ya sasa


Paroles2Chansons dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)