Bomba Ipepee
Manengo
paroles Manengo Bomba Ipepee

Manengo - Bomba Ipepee Lyrics & Traduction

Na nisipotoka sio tu Mungu mpaka shetani ata doubt
Warrup, tumia akili kabla haijakutumia
Manengo, you know me
Stamina, you know me
Busy, busy, busy, lets Go!

Okey, niko peke yangu, sina dada wala ndugu
Wakinitaka nipo baa nakunywa Pombe Magufuli
Gigi kunipa papa, mliona wivu ka napanda ndwafu
Waambieni nipo Kenya napewa Papa Jones na Khaligraph(Mschew)

Waambieni watoto warudi shule 
Nawashangaa wanauza K wakati Mwanza zihuwa bure
Saa, kanikimbia Mwanza kaenda Tambora kaliwa
Chungeni msicheze Iokote gerezani mtalia

Mi ni Yanga, nampiga mdogo na mkubwa yaani
Namkalisha danda mpaka simba wa Yuda
Similiki dem, similiki shem 
So ukiniona ninajichua jua nina maumivu sehem

Picha ya Mjoni, so hamjui ata kusoma 
Kwa manengo wamecheka na mla mhindi wa kuchoma
Na sio Bongo tu, nenda Mozambique watakwambia kuwa 
Nauza chai ya rangi, ubongo maziwa

Kama jahazi linasonga
Wacha bomba ipepee, wacha bomba ipepee
Mpaka tuna tia nanga, wacha bomba ipepee
Wacha bomba ipepee

Watoto wamejiroga
Kimya na kuguza guza soda
Watu wazima cheki tunavuka boda
Watu wazima cheki tunavuka boda

Ah, na huu mwaka nawachezesha kichura chura
Kikuta napiga tano, cargonini huko manura
Pole mnafiki Mr Yuda, mbele yangu huwezi tamba
Naona unapoteza muda ka mshenga wa Dogo Njanja

Wanaonijua vizuri hawana shaka na mimi
Wanadata na mimi, nikitema wanadaka madini
Mtu makini, mchezoni mi huuza sura kwa nini?
Ngumu kumeza, Mr Paka roho saba kazini

Ukiona anatingisha kichwa, cheki na zipu
Maana nina vichwa viwili navyo tumia kila siku
Waambieni wapizani, habari yao tunayo 
Wasije CCM kirhumba, watapigwa roba za mbao

Shoga ukikosa vumba, danga 
Kuhusu bikogo ya mapenzi pata mchumba, Tanga
Ah kula sana unga, wanga
Ukipata dem kisu tafta chumba, manga 

Kama jahazi linasonga
Wacha bomba ipepee, wacha bomba ipepee
Mpaka tuna tia nanga, wacha bomba ipepee
Wacha bomba ipepee

Watoto wamejiroga
Kimya na kuguza guza soda
Watu wazima cheki tunavuka boda
Watu wazima cheki tunavuka boda

Nina mistari nidhamu, tega sikio niwaonyeshe
Yaani mi ni mtamu, mpaka Nandy aliniomba nimnogeshe
Manengo ni chuo bro na sio veta
Napigaga guitar, kinanda hadi zezeta

Waambieni watabiri wa ndoto, mi hizi ndoto zinanionea
Maana nikilala na mto huwa naotaga naogelea
Na ununda wangu wote, sijawai kwenda segerea
Ghetto navuta subira, kuliko powder na mmea

Mi nimeshazoea ng'ombe na mbuzi nusu
Kwa hiyo siridhishwi na dem mwenye kikuku 
Msichojua, kwenye collabo, namkalisha mkali wao 
Mkuje simba, paka na mkali wenyu

Kuhustle ndo kauli mbiu, amkeni washikaji
Unaeza ukafa na kiu na huku unakaa ubongo maji
Nilikotoka ni hatari, hakiombeki hali mbaya
Hata nikifa bila gari, nitaendesha huko Galilaya

Kama jahazi linasonga
Wacha bomba ipepee, wacha bomba ipepee
Mpaka tuna tia nanga, wacha bomba ipepee
Wacha bomba ipepee

Watoto wamejiroga
Kimya na kuguza guza soda
Watu wazima cheki tunavuka boda
Watu wazima cheki tunavuka boda

Lazima cheki tunavuka boda
Bomba ipepee, acha bomba ipepee
Ooooh wooh, acha bomba, acha bomba
Tumia akili kabla haijakutumia


Paroles2Chansons dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)