Nieleze
Ibrah Nation
paroles Ibrah Nation Nieleze

Ibrah Nation - Nieleze Lyrics & Traduction

Ona nguvu zimeniisha
Ghafla nimekua bubu
Kama mtoto najiliza
Nifute chozi malikia wangu
Kulikosa penzi lako shida
Napata homa
Unanifanya nichukie mapenzi
Nayaogopa

Au sababu mchizi anahudumia
Hajakupenda kweli anakutumia
Yuko na wewe na nyumbani ana mke pia
Hunitaki single boy yoh nami na moyo

Mamy nieleze, nieleze
Niendelee kusubiri
Au nafsi najikatili mimi
Mamy nieleze, nieleze
Niendelee kusubiri
Au nafsi najikatili mimi

Ouuhhhhh… yeah

Kwenye basi lako mi ndio abiria
Ukinishusha njiani utanionea
Mi nashambuliwa maradhi naugulia mwenyewe
Kwenye basi lako mi ndio abiria
Ukinishusha njiani utanionea
Mi nashambuliwa maradhi naugulia mwenyewe
Mpaka natamani upofu
Macho yangu yasikuone
Moyo unachomwa mwiba
Nikikuona unatoka na yeye

Au sababu mchizi anahudumia
Hajakupenda kweli anakutumia
Yuko na wewe na nyumbani ana mke pia
Hunitaki single boy yoh nami na moyo

Mamy nieleze, nieleze
Niendelee kusubiri
Au nafsi najikatili mimi
Mamy nieleze, nieleze
Niendelee kusubiri
Au nafsi najikatili mimi

Hata siwezi kusonga
Mbele naona jau
Eti nikimbie kinyonga
Mbona nimaajabu
Ndio ivo tena apeche alololo
Labda nitapataga tomorrow
Nikupe Magari ya kifahari
Na nyumba Morogoro

Ringtone on the beat


Paroles2Chansons dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment