Nikumbushe Wema Wako
Angel Benard
paroles Angel Benard Nikumbushe Wema Wako

Angel Benard - Nikumbushe Wema Wako Lyrics & Traduction

Halleluyah
Oooh ooh eeh
Halleluyah

Nirahisi kinywa kujawa na lawama tele
Pale mambo yanapoonekana hayaendiii
Ni ajabu sana, namna moyo unahangaika
(Kutafuta majibu)

Ajabu sana moyo unavyoonyesha mashaka 
Yakwamba japokuwa Mungu anaishi ndani yangu 
Kuna muda nahofu 
Japokuwa Mungu anaketi kati yetu 
Kuna muda nahofu,

Oooh nakumbuka wana wa Israel 
Katika bahari ya Shamu 
Japo walikatiza 
katikati ya bahari kwa ushindi

Kwa nyimbo nyingi 
Waliimba na kumsifu Bwana 
Lakini baada ya kuvuka na kuliona jagwa
Yalibadilika mambo

Manung'unikoo yalisimama 
Na kusahau muujiza alotenda Bwana mwanzo(Aah)
Eee MUNGU 
Niisaidieee eee eenhee

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Eeeh Ee MUNGU Nisaidiee

Nisaidieee
Kukumbuka baba 
Yakwamba umenichora 
Kiganjani mwako 

Kati ya wengi waliopo duniani eeh
Na mimi umenionaa oooh ooo
Nikumbushe baba 
Yakwamba ni wewe umeniponya nilipoumwa
Yakwamba ni wewe mlipaji wa ada yangu shuleni oooh
Yakwamba kama ungeniacha hatua moja 
Nisingelifika nilipo ooh eee Babaaa

Umenikung'uta mavumbi
Kung'uta mavumbi mimi na kuniheshimisha
oooooh oooooh

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Eeeh Ee MUNGU Nisaidiee


Paroles2Chansons dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)