paroles Annastacia Mukabwa Dawa

Annastacia Mukabwa - Dawa Lyrics & Traduction

Hehehe kuna watu wenye majina
Lakini walipokufa walisahauliwa
Lakini jina la Yesu ni jina la kipekee
Usisahau kuita jina la Yesu kila wakati

Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Eeh ni dawa, jina la Yesu ni dawa
Nasema ni dawa tosha, jina la Yesu ni dawa 

Dawa inayosamehe dhambi, jina la Yesu ni dawa
Eeh ni dawa yoh yoh, jina la Yesu ni dawa
Ni jawabu la maisha, jina la Yesu ni dawa
Natangazia ulimwengu wote jina la Yesu ni dawa

Wacha niseme, 
Mungu kauliza kwenye kiti cha enzi
Kikao kilipokaa kule mbinguni
Nani atakwenda mbinguni amwokoe mwanadamu

Malaika wote walinyamaza kimya
Wazee ishirini na nne walinyamaza kimya
Yesu mwana wa Mungu akasema nitakwenda
Kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi

Akafa kifo cha aibu kwa ajili yangu na wewe
Alipigwa akadhulumiwa kwa ajili yangu na wewe
Mungu alipo tazama hilo ee Baba
Akasema amejitoa kwa ajili ya wanadamu

Nimempatia heshima na jina la heshima
Unapotaja jina la Yesu unafunguliwa
Unapotaja jina la Yesu unawekwa huru

Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Yabadilisha wenye dhambi, jina la Yesu ni dawa
Limebadilisha na majambazi, jina la Yesu ni dawa
Yabadilisha makahaba, jina la Yesu ni dawa 

Yabadilisha walevi eh, jina la Yesu ni dawa
Jina la Yesu ni dawa, jina la Yesu ni dawa
Iiii ni dawa , jina la Yesu ni dawa
Iiii ni dawa , jina la Yesu ni dawa

Naona watu wanatembea kwenye giza
Wana macho lakini hawaoni
Wana masikio lakini hawasikii
Wanahangaika, wanahangaika

Wanatafuta msaada kwa karumazira
Vijana wadogo wanatafuta masponsa
Hello, hello, mnisikie
Yesu leo ameinuliwa kama nyoka wa shaba

Nami leo naliinua jina la Yesu
Kwa jina hili viwete wanatembea yoh yoh
Kwa jina hili vipofu wapata kuona
Kwa jina hili tumepata imani sisi

Kwa jina hili tumepata imani sisi
Kwa jina la Yesu leo ah tumemwona Bwana
Kwa jina la Yesu leo tumeinuliwa
Kwa jina la Yesu leo tumesamehewa dhambi

Kwa jina la Yesu leo tunaitwa wana wa Mungu
Kwa jina la Yesu leo twamtumikiwa Bwana
Kwa jina la Yesu eeh jina lenye nguvu
Jina hili ni power, jina hili ni moto

Jina hili ni nguvu eey, kiboko ya wachawi
Wanapolisikia yeye wanasurrender wenyewe
Jina hili Yesu wee, limetubadilisha 
Jina hili Yesu wee, limetuinua baba

Jina la Yesu wapendwa limetutengeneza
Tulikuwa hatuna maana limetuosha
Tulikuwa twadharauliwa tumepata heshima
Jina la Yesu wapendwa ni dawa tosha
Wagonjwa mnisikie dawa ni Yesu wee

Aah Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Aah ni dawa yeah yeah, jina la Yesu ni dawa
Hata kwa taifa langu, jina la Yesu ni dawa
Waimbaji twalitegemea, jina la Yesu ni dawa 

Kwa kanisa ni dawa tosha, jina la Yesu ni dawa
Hata kwa wanasiasa ni dawa, jina la Yesu ni dawa
Eeeh, jina la Yesu ni dawa
Eeeeh, jina la Yesu ni dawa

Dawa dawa dawa dawa
Dawa dawa dawa dawa


Paroles2Chansons dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)