Darasa La Saba
Mbosso
paroles Mbosso Darasa La Saba

Mbosso - Darasa La Saba Lyrics & Traduction

Mwishoni darasa la saba mi naye ndio tulijuana
Sababu ya kukosa ada mi kidato ikashindikana

Ndoto za udaktari kwisha habari zikapeperuka
Na yeye sekondari akahamishwa mbali mkoani Arusha
Hisia na balehe zilikutana kati mambo ya kupenda
Ujana maji ya moto eh moyo ngoja basi
Nikaja kuskia yuko Gongo la Mboto
Mara chuo Mtwara Masasi
Nyie wahenga waongo kwamba dunia ndogo
Mbona sijui sasa yupo wapi

Namtafuta bado namtafuta mchumba wangu wa darasa la saba
Ajue sikuchezea fursa ni wazazi walikosa ada
Bado namtafuta mchumba wangu wa darasa la saba
Ajue sikuchezea fursa ni wazazi walikosa ada

Tere rireh tere sanaam
Tere rireh tere sanaam
Tere rireh tere sanaam
Tere rireh tere sanaam

Mara ya mwisho kumuona ni siku ya mahafali
Niliandika ujumbe ila hakuusoma nyuma ya daftari
Suluhisho mi kupona nijue angali mzima
Yupo salama niache kusonona moyo upate afadhali
Nikimuona nitamsimulia yote niliyoyapitia
Ajue yeye ndiyo chanzo cha mimi kuishi duniani
Nilivyommiss nitakumbatia huenda naye kanimiss pia
Ni mawazo yanayonizunguka kichwani

Ndoto za udaktari kwisha habari zikapeperuka
Na yeye sekondari akahamishwa mbali mkoani Arusha
Hisia na balehe zilikutana kati mambo ya kupenda
Ujana maji ya moto eh moyo ngoja basi
Nikaja kuskia yuko Gongo la Mboto
Mara chuo Mtwara Masasi
Nyie wahenga waongo kwamba dunia ndogo
Mbona sijui sasa yupo wapi

Namtafuta bado namtafuta mchumba wangu wa darasa la saba
Ajue sikuchezea fursa ni wazazi walikosa ada
Bado namtafuta mchumba wangu wa darasa la saba
Ajue sikuchezea fursa ni wazazi walikosa ada

Tere rireh tere sanaam
Tere rireh tere sanaam
Tere rireh tere sanaam
Tere rireh tere sanaam

Paroles2Chansons dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)